No new announcemente


  JIFUNZE TECHNOLOGY
User Avatar Forum: Technology
Posted by: dau1996 - 03-01-2018, 09:56 PM - Replies (1)

MAPINDI NDO YANAANZA JIUNGE SASA KWENYE CHANNEL YA TELEGRAM UPATE MAUJUZI.

TUNATAKA WENGI WAJUE UTUMWA UISHE WA TEKNOLOJIA.

NI BURE HAUCHAJIWI LABLA VITU VIDOGOVIDOGO.

TUMEANZA SASA USIKU NJIA YA KWANZA .

HALI NI NGUMU KAZINI TUNARUDISHWA ILA SMATPHONE YAKO,COMPUTER YAKO INA PESA ILA WEWE HAUFAHAMU.

JE UNAZIFAHAMU NJIA 65 ZA KUPIGA PESA MTANDAONI KM HUZIFAHAMU KARIBU UZIFAHAMU.

NI BUREEE HUTOZWI ILA KM HUTAKI FANYA KM MDOMO WAKO UNAUFUNGA ZIPU YAANI NYAMAZA.

DOWNLOAD TELEGRAM JISAJILI THEN SELECT LINK HII UJIUNGE

https://t.me/joinchat/AAAAAD_WkgQsOKJjsYvfWQ

ILA KM HUTAKI KUJIUNGA KAUSHA COZ KUNA ASILIMIA YA WATU HAWA SIO WATU TUWAWEKE KWENYE KUNDI LA MIMEA WANAJUA KUPONDA KULIKO KUJENGA.

WENZETU WANAENDELEA SISI TUMEBAKIA KUPONDA TU.

KM UNAPENDA UJUZI JIUNGE LINK NAWEKA TENA

https://t.me/joinchat/AAAAAD_WkgQsOKJjsYvfWQ

Sent from my PHANTOM5 using Tapatalk

Print this item

  Wasafi tv&radio
User Avatar Forum: Celebrities and superstars
Posted by: Rover - 03-01-2018, 05:18 PM - Replies (2)

Diamond aitambulisha wasafi tv & radio Zanzibar.
Msanii maarufu nchini wa muziki wa kizazi kipya, Abdul Nasib au Diamond amesema lengo la kuanzisha vituo hivyo ni kutoa ajira kwa vijana hasa waandishi na watangazaji ambapo amewataka kuitumia fursa hiyo itakayowasaidia katika kuondokana na tatizo la ajira linaloikabili Tanzania.Attached Files Thumbnail(s)
   
Print this item

  Utegemezi
User Avatar Forum: Je wajua (did you know)? .now you know
Posted by: Taita - 03-01-2018, 04:25 PM - Replies (1)

Kwa hali kama hii kweli tutafanikiwa kufikia uchumi wa viwanda?Attached Files Thumbnail(s)
   
Print this item

  Msaada
User Avatar Forum: Habari na mada mbalimbali
Posted by: Rover - 03-01-2018, 10:56 AM - Replies (4)

Habari wakuu
Naombeni msaada wa kisheria au mawazo, nimeachana na mke wangu kwa matatizo ya kifamilia yaliyotokea, sasa mwanamke kaenda mahakamani anataka tugawane mali tulizonazo. Ieleweke ndoa tulifunga kwa imani za kiislam na kufuata sheria za kiislam na tumeishi katika misingi ya kiislam na hata kuachana tumefuata taratibu za kiislam. Sasa katika uislam mwanamke akitaka yeye kuachika, huwa hapati chochote kutoka kwa mume kama haki yake, labda huyo mume aamue tu kumpa chochote lakini sio lazima. Sasa huyu mwanamke yeye ndio alietaka kuachika na talaka akaandika yeye mimi nikaisaini. Sasa kaenda mahakani anadai tugawane mali. Hapo sheria inasemaje wakuu, maana mi ndoa sikufunga mahakani wala serikalini, mahakama inawezaje kuingilia swala la imani? Na imani hiyo sote wawili tulikubali masharti na taratibu zake za ndoa na mengine yote? Naomba mawazo wakuu

Print this item

  Maandamano
User Avatar Forum: Habari na mada mbalimbali
Posted by: Rover - 02-28-2018, 09:52 PM - Replies (1)

Watanzania waishio nchini ujerumani hatimae wapewa kibali cha kufanya maandamano ya kupinga mambo yanayofanyika nchini Tanzania.Attached Files Thumbnail(s)
   
Print this item

  Tanzania yangu
User Avatar Forum: jukwaa la siasa
Posted by: Rover - 02-28-2018, 02:11 PM - Replies (2)

Habari wakuu
Niende moja kwa moja kwenye mada, Tanzania yetu ni nchi ya amani sana, hilo tunajivunia katika dunia yetu hii, lakini kwa sasa wanasiasa wanataka kutuvurugia, nchi nyingi duniani hazina amani kutokana na siasa/wanasiasa, watanzania tusikubali kufika huko, ni jukumu la viongozi wetu wakuu kuliangalia hili kwa namna ya pekee. Vyombo vya habari vipaze sauti na kuendesha mijadala ya kutafuta suluhu, na ili kupata suluhu mijadala iendeshwe kwa viongozi wa dini na wataalamu wa maswala ya usalama. Hii mijadala inayoendeshwa na wanasiasa wenyewe haiwezi kupatikana muafaka kwa sababu kila mwanasiasa anavutia kwake na kujisifia yeye ni bora kuliko mwingine (chama). Tanzania yetu ni muhimu kuliko vyama na wanasiasa.

Print this item

  Mwanaume mgeni hukaribishwa kwa tendo la ndoa
User Avatar Forum: Habari na mada mbalimbali
Posted by: Singa1 - 02-27-2018, 08:30 PM - Replies (1)

Fahamu kabila la ‘Ovahimba’ ambalo mgeni hukaribishwa kwa kushiriki tendo la ndoa

Wakati dunia nzima ikipambana kuzuia ongezeko la maambukizi ya magonjwa ya ngono kama UKIMWI, Kaswende, Gonorea na magonjwa mengine yanayoshabihiana, hii ni tofauti kabisa na kabila la OVAHIMBA ambalo hadi karne hii ya 21 bado wanatamaduni hatari kwa afya zao.

Kabila la OVAHIMBA ambalo linapatikana kaskazini mwa Namibia katika mikoa ya Kunene na Omusati, bado wanautamaduni wa kuwapokea au kuwakaribisha wageni wa kiume kwa kufanya mapenzi wakiamini kuwa hiyo ndiyo heshima anayostahiri mgeni.

Imeelezwa kuwa mgeni anapowasili kwa siku ya kwanza kama ilivyokawaida huandaliwa chumba na kisha kumteua mwanamke/binti ambaye hajaolewa kwenye familia kulala na mgeni kitanda kimoja kwa siku ya kwanza.

Na kama kwenye familia aliyofikia mgeni hakuna mwanamke ambaye hajaolewa basi wanaume kwenye familia hiyo hupiga kura ili mmoja wao kumuachia mgeni chumba chake alale na mkewe.

Kama mwanaume huyo nyumba yake itakuwa na chumba kimoja na sebule basi atamuachia mkewe alale na mgeni chumbani kwake.

Kwa maelezo ya makala iliyochapishwa na mtandao wa shirika la habari la AP, imeelezwa kuwa wanawake huwa hawana njia ya kukataa maamuzi hivyo moja kwa moja hutii maamuzi ya wanaume kwenye jamii yao.

Kwa wageni wa kike hao huachwa walale na watoto na huwa hawafanyiwi chochote.

Kabila hilo ambalo linaamini mpaka sasa kifo kama wanavyoita wenyewe ‘Omtiti’ husababishwa na wachawi kwenye jamii hizi.

Asubuhi mwanamke ambaye amelala na mgeni hukaguliwa kama alishiriki tendo la ndoa na kama hakushiriki huongezewa usiku mwingine.

Kabila la Ovahimba wanaamini kuwa mwanaume yeyote hutembea na bahati, hivyo kwa kulala na mwanamke aliyekwenye familia yao huongeza bahati.

Kwa sensa ya mwaka 2010 kabila hilo lilikuwa na watu 50,000 na tayari serikali nchini Namibia imepanga namna ya kuiokoa jamii hiyo ya wafugaji ambayo inaishi karibia na jangwa la Namib.

Kwa upande mwingine kabila hilo wasichana huchaguliwa na baba zao wanaume wa kuwaoa na mahari huwa ni ng’ombe na asali.        

Sent from my Infinix HOT 4 Lite using Tapatalk

Print this item

  Mwanamke wa kwanza kuendesha ndege ya kivita nchini India
User Avatar Forum: Habari na mada mbalimbali
Posted by: Singa1 - 02-27-2018, 07:00 PM - No Replies

Avani Chaturvedi, 24, amekuwa mwanamke kwa kwanza kuendesha ndege ya vita akiwa peke yake nchini India.

Aliendesha ndege ya Mig-21 Bison kwa dakika 30 mapema wiki hii, kwa mujibu wa jeshi la wanahewa la India.

"Aliitaja siku hiyo kuwa ya kihistoria katika jeshi la India, msemaji Anupam Banerjee aliiambia BBC.

   

Sent from my Infinix HOT 4 Lite using Tapatalk

Print this item

  Watu 7 wafariki Nigeria,baada ya msichana mkristo kuwa muislamu
User Avatar Forum: Habari na mada mbalimbali
Posted by: Singa1 - 02-27-2018, 06:54 PM - Replies (2)

Takriban watu saba wameuawa katika vita ambavyo vilizuka baada ya msichana wa dini ya Kikristo kubadili dini na kuwa Mwislamu Kaskazini magharibi mwa Nigeria.

Vita hivyo vilivyozuka katika jimbo la Kaduna viliwaacha watu 15 wakiwa na majeraha baada ya nyumba kuchomwa moto.

Shahidi mmoja aliambia BBC kwamba tatizo lilianza baada ya msichana huyo wa Kikristo kutoka Gwari kubadili dini na kuwa Muislamu kutokana na ushawishi wa mpenzi wake.

Shahidi anasema kuwa tatizo hilo liliwachochea vijana wa Kikristo .

Ripoti nyengine zinasema kuwa wasiwasi kati ya wafuasi wa dini hizo mbili ulikuwa tangu awaliSent from my Infinix HOT 4 Lite using Tapatalk

Print this item

  Chelsea vs Barcelona live
User Avatar Forum: Michezo
Posted by: Singa1 - 02-21-2018, 12:05 AM - Replies (2)

Kama hukupata kwenda kibanda umiza,basi click link hi pakua app ya Tuzungumze forums kisha open na tazama game.
online....pakua hii https://play.google.com/store/apps/detai...ungumzecom

Sent from my Infinix HOT 4 Lite using Tapatalk

Print this item