No new announcemente


BABA WA MAYWEATHER AMPIGA MWANAMKE
  • 4 Vote(s) - 3 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5

#1
Baba wa bondia Floyd Mayweather Jr, amekamatwa na Jeshi la Polisi la Las Vegas nchini Marekani akituhumiwa kumshambulia kwa masumbwi mwanamke mwenye umri wa miaka 59.

Kwa mujibu wa taarifa za polisi, mzee Mayweather anatuhumiwa kumpiga mwanamke huyo Septemba mwaka jana walipokuwa wanatoka kushuhudia pambano na masumbwi kati ya Canelo Alvarez na Gennady Golovkin.

Afisa wa jeshi hilo, Aden OcampoGomez amesema kuwa mwanamke huyo alifungua jarada Septemba 17 mwaka jana akieleza kuwa aliingia katika ugomvi wa majibishano ya maneno kati yake na mzee huyo katika eneo la maegesho ya magari ndipo alipomvuta kutoka kwenye gari lake na kuanza kumshambulia kwa masumbwi.

Mwanamke huyo alipelekwa hospitalini na akapatiwa matibabu ya majeraha hasa michubuko aliyoipata katika ugomvi huo.

Mzee Mayweather ambaye aliwahi kuwa mpiganaji wa masumbwi na sasa ni mkufunzi, alishikiliwa na jeshi hilo Jumatano wiki hii na aliachiwa kwa dhamana ya $1,000 akisubiri kupandishwa kizimbani Machi 27.

Endapo atakutwa na hatia kwa mujibu wa sheria, mzee huyo mwenye umri wa miaka 65 atakumbana na kifungo cha miezi sita jela.[Image: 0a11d1f2d07ca4594d7bb38c7b7bd916.jpg]
Reply
#2
Mtot miaka 59 baba 65???🚎

Sent from my Infinix HOT 4 Lite using Tapatalk
Reply
#3
Mwanamke aliepigwa ndio ana miaka 59
Reply
#4
Ninavyojua mawe (ngumi)ya huyo mzee, huyo mama nahisi kapata michubuko kwa sauti tu ya majibizano, maana mzee akishusha jiwe 1 tu kwa mama asiekuwa na zoezi lazima azame ardhini, kinachofuata ni kufukia tu
Reply
#5
Huyu mleta uzi huyuu kwa kuipamba sasa...


Sent from my iPhone using Tapatalk
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)