No new announcemente


YANGA SC
  • 5 Vote(s) - 3.4 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5

#1
YANGA INAKULA MATUNDA YAKE 

Moja ya vikosi vya Yanga SC vilivyowahi kutikisa anga la soka Tanzania na Afrika mashariki ni miaka miongo miwili nyuma,miaka ya 1993, 1994-1995 , 1998 na 1999 katika orodha ya majina ya vikosi hivyo ni lazima utaliona jina la beki kisiki Keneth Mkapa. 

Keneth Mkapa anakumbukwa sana kwa ubora wake kama mlinzi wa pembeni akishiriki vyema katika kikosi bora cha Yanga SC cha mwaka 1993 ligi ya klabu bingwa Afrika mashariki na kati ( hivi sasa Kagame Cup ) kilichobeba kombe hilo nchini Uganda baada ya kuwalaza majogoo wa soka nchini Uganda Sports Club Villa kwa magoli 2-1 huku marehemu Saidi Mwamba Kizota akiibuka mfungaji bora wa mashindano , Mkapa mlinzi bora wa kushoto huku kinda ( wakati huo ) Edibily Lunyamila akisimama kama mchezaji bora chipukizi wa mashindano akiacha gumzo la aina yake. 

Kikosi kamili kilikuwa hivi ;
1. Steven Nemes/Rifat Said ( Marehemu )
2. Mwanamtwa Kihwelu
3. Keneth Mkapa
4. Willy Mtendamema
5. Issa Athuman ( Marehemu )
6. Method Mogella ( Marehemu )
7. Zamoyoni Mogella
8. Steven Mussa/Hamis Thobias ‘gagarino’ (wote ni Marehemu )
9. Said Mwamba ‘kizota’ ( Marehemu )
10. Mohamed Husein ’Chinga’
11. Edibily Jonas Lunyamila

-Willy Martin, 
-Rifat said, 
-Aboubakar salum "sure boy" 
-David Mwakalebela "MP" 

Keneth Mkapa , Lunyamila, Mmachinga na wengineo licha ya kustaafu soka zaidi ya miaka kumi iliyopita lakini bado wameendelea kuwa na mchango mkubwa kwa klabu yao pendwa wakiipa sapoti katika mambo mbalimbali likiwemo la ushauri kiufundi na kusimamia maadili , desturi na tamaduni za klabu hiyo kwa wachezaji chipukizi na vijana ambao wana kiu ya kuitumikia klabu hiyo. 

Hivi sasa Yanga ipo katika mchakato wa kusaka vipaji kwa vijana chini ya umri wa miaka 17 na wakongwe hawa ndio wanaendesha zoezi hili ili kupata vijana wenye vipaji sahihi, nidhamu binafsi na nidhamu ya mpira ambayo itawafanya kuitumikia vyema klabu hiyo. 

Mfumo huu wa kutumia magwiji wa klabu hiyo ambao walicheza kwa mafanikio ni kama Yanga inakula matunda yake yenyewe na kuimarisha ustawi wa klabu hiyo kimbinu, kiufundi, falsafa pia desturi. 

Vijana hao wadogo ambao watafaulu katika mchakato huo na kuelezwa vyema historia za watahini wao ni dhahiri hali hiyo itawapa mtaji mzuri wa kisaikolojia katika kujibidiisha ili kujaribu au kupita historia za wandamizi hao. 

Pichani chini ni Keneth Mkapa akiwafanyia usaili vijana wanaotaka kujiunga na Yanga kids.
Reply
#2
Yanga timu hatari saana mpka tukawaita wa kimataifa,mtu unashinda kombe la ligi mara 4 mfululizo sio mchezo,utafikiri nchi hi timu hamna ,inacheza yenyewe
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)