No new announcemente


English
  • 4 Vote(s) - 4.25 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5

#1
Psite Shio:
Somo la 1

(SECTION A; TENSES IN THE ACTIVE VOICE )

(A)Simple Tenses :

1. Simple Past Tense ( ‘li’)
- Wakati huu huongelea jambo lililofanyika na kukamilika mara moja wakati uliopita.
Mifano ; tulikuja ,walitembea, alicheza.
- Wakati huu huashiriwa na silabi ‘li’ ambayo hufanya tutambue kuwa tunaongelea jambo lililofanyika mara moja na likamalizika kufanyika katika wakati uliopita. Hii silabi ‘li’ ni lazima iunganishwe na kitendo moja kwa moja kabla ya kitendo. Mfano ; ‘Tuliimba’, tofauti na ‘Tulikuwa tunaimba’ ambapo ‘li’ imefuatiwa na kifungu ‘kuwa’ na sio kitendo. Katika maneno ‘tulikuwa tunaimba’, kitendo ‘imba’ kimetanguliwa na ‘na’ na sio ‘li’ kwa hivyo maneno hayo hayapo katika wakati huu wa Simple Past Tense, ‘li’.

Kanuni za kutumia Simple Past Tense ‘li’

a) Sentensi za taarifa/kutoa taarifa
Katika wakati huu, huwa tunapoelezea jambo tunatanguliza mtendaji wa jambo, (I/We/You/They/He/She/It) kisha tunafuatisha kitendo moja kwa moja kikiwa katika umbo la wakati uliopita.
Mfano ; - kitenda ‘enda’ ni ‘go’. Umbo lake la wakati uliopita, yaani ‘-lienda’ ni ‘went’. Tutatanguliza mtendaji wa jambo kisha tufuatishe neno ‘went’.

Sentensi za mifano;
- Juma alienda. ………. Juma went.
- Tulienda. ……… We went.
- Basi liliondoka. ……. The bus left.
- Nilicheza. ……. I played.
- Uliimba. ….. You sang.
- Walikimbia. ….. They ran.
- Maria alipika. ……. Maria cooked.
NB : Hatuweki kitu chochote katikati mwa mtendaji na kitendo.

b) Kuuliza maswali katika Simple Past Tense

- Maswali katika wakati huu huanzia na neon ‘did’. ‘Did’ ikitumika ni lazima kitendo kiwe katika umbo la kawaida kwa sababu ‘did’ ina ‘li’ ndani yake hivyo ‘li’ nyingine haihitajiki. Ina maana hiyo ‘did’ tayari imeshawakilisha wakati uliopita.
- ‘Did’ hufuatwa na nafasi inayouliziwa swali.
Mifano ya tafsiri :
- ‘Did Juma _ ?’ …….. ‘Je, Juma ali____?’
- ‘Did they _ ?’ ………. ‘Je, wao wali____ ?’

Sentesi za mifano :

1. Did Juma go?
Je, Juma ali enda ?

Jibu ; ( Hapana, hakuenda)…..( Kukanusha)
No, he didn’t go.
Au ; ( Ndio, alienda)…. Kukubali
Yes, he went.

2. Did she cook?
Je, alipika?

Jibu ; ( Hapana, hakupika)…..Kukanusha
No, she didn’t cook.
Au ; Ndio, alipika….. (Kukubali)
Yes, she cooked.

** katika kitabu kuna michoro ambayo inaonyesha tafsiri ya moja kwa moja ya kila kipengele cha sentensi kutoka kiswahili hadi kingereza ila hapa hatujaionyesha.

NB ; Tukiongeza neno ‘did’ katikati mwa jibu la kukubali, huwa ni kuweka msisitizo kama vile ambavyo kwa Kiswahili huwa tunaandisha sauti ili kuweka msisistizo ila sasa kwa Kingereza sauti haipandishwi ila msisitizo upo pale pale.

Mifano ; 1. Did Juma go ? …… Je, Juma alienda?
- Yes, he did go. ….. Ndio, alienda! (KWA MSISITIZO)

2. Did they cook? …….. Je, walipika?
- Yes, they did cook. …… Ndio, walipika! (KWA MSISITIZO)

NB ; Tunapokanusha sentensi kwa kutumia ‘did not’/ ‘didn’t’ , huwa hatutumii kitendo kikiwa katika umbo la wakati uliopita maana ile ‘did’ inakuwa imeshawakilisha wakati uliopita (‘li’ ambayo kinume chake ni ‘haku’) kwa hivyo hatuhitaji wakati uliopita kwa mara ya pili. Tukitumia umbo la wakati uliopita pia kwa kuuliza swali lililoanzia na ‘did’ pia tunakuwa tumeweka ‘li’ mbili katika sentensi, jambo ambalo sio sahihi.

Mifano ; 1. She didn’t went yesterday. ( Badala ya ‘She didn’t go yesterday.’)
Haku lienda jana. ( Badala ya ‘Hakuenda jana.’)

Au; 2. Did she went yesterday?
( Badala ya ‘Did she go yesterday?’)

- Je, yeye ali lienda jana?
( Badala ya ‘Je, yeye alienda jana?)

Sent from my NokiaX2DS using Tapatalk
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)