No new announcemente


Amber Lulu atoa mimba ya Prezzo
  • 8 Vote(s) - 3.88 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5

#1
KAMA mjuavyo siku zote kwamba ili ubuyu unoge ni vizuri tuumung’unye tukiwa wengi, peke yako haonogi bwana na ndio maana ‘nashea’ na nyinyi kila wiki kupitia safu hii ya Ubuyu.  Kwa leo nawaletea ubuyu wa aliyekuwa muuza nyago maarufu ambaye kwa hivi sasa amegeukia kwenye muziki, Lulu Auggen ‘Amber Lulu’ anayetamba na wimbo wa Jini Kisirani. 

Kwa nini ametupambia Ubuyu wa leo mrembo huyu? Anadaiwa kuchoropoa mimba ya mwanamuziki maarufu nchini Kenya Jackson Makini ‘Prezzo’ wakati ujauzito huo ukiwa umeshaanza kuwa mkubwa. 

TUJIUNGE NA CHANZO 
Mpashaji wetu ambaye ni rafiki wa karibu na Amber, alishusha ‘vesi’ kuwa, mrembo huyo kuna kipindi alikaa sana nchini Kenya kwa mpenzi wake huyo na hata aliporejea Bongo, alikuja mara mojamoja na kuondoka. 

Mnyetishaji huyo aliendelea kumwaga mchele kwenye kuku wengi kwa kusema kuwa, kutokana na kuja huko kwa ‘wiziwizi’ ilikuwa ni vigumu hata kwa watu kujua kama amenasa ujauzito huo huku ikidaiwa, Prezzo alishaamua kuishi naye kabisa kama mtu wake na baadhi ya ndugu zake wa karibu walishaanza kumjua. 

“Unajua kuna kipindi Amber Lulu alikuwa hayupo kabisa nchini aliporejea alikuwa tayari na ujauzito lakini hakuna mtu aliyeweza kumgundua kwa haraka kwa sababu alikuwa akikaa kidogo sana na kuondoka labda watu wake wa karibu tu ndio walikuwa wakijua maana mwenyewe alifanya siri kubwa hakupenda watu wajue akihofia pia angeweza kukosa shoo mbalimbali,” alisema sosi huyo mwaminifu. 

 Chanzo hicho kilizidi kuweka wazi kuwa, si mashabiki tu aliowaficha, hata baba kijacho mwenyewe Prezzo hakumueleza kuhusu ujauzito wake huo kwa sababu kuna kipindi walikuwa hawako sawa hivyo aliona isije akamweka wazi halafu akamuacha kwenye mataa kitu ambacho asingekipenda kitokee na ukizingatia maisha yake anategemea muziki. 

“Unajua Amber alipopata ujauzito huo nahisi alikuwa hana maelewano mazuri na Prezzo akaona amfiche kwanza kusikilizia kama wataelewana. Akimueleza kama amebeba ujauzito wa mwanamuziki huyo na kamtolea nje itakuwa ni shida sana huku yeye mwenyewe anategemea muziki kuendesha maisha yake,” kilisema chanzo. 

HUYU HAPA AMBER LULU 
Baada ya gazeti hili kupata ubuyu huo, lilimtafuta Amber Lulu ili aweze kufafanua madai hayo mazito ambapo alipobanwa maswali alifunguka kama ifuatavyo: 

Wikienda: Vipi Amber, mbona nilisikia una ujauzito wa Prezzo? 

Amber: Nani amekwambia maana ungeniona hapa na kitumbo. 

Wikienda: Nasikia uliichoropoa hukutaka kero. 

Amber: Kero ya nini sasa maana mimba ningebeba mimi lakini siyo yeye (Prezzo). 

Wikienda: Kwa hiyo bado mko kwenye uhusiano na Prezzo? 

Amber: Ndio niko naye bado na kuhusu kushika ujauzito siku si nyingi. 

Wikienda: Sasa si ulipata ukatoa? 

Amber: Mimi sitaki kuzungumzia hiyo habari bwana na wala sitaki uiandike. 

Wikienda: Haya nashukuru sana Amber. 

Amber: Asante. 


Sent from my Infinix HOT 4 Lite using Tapatalk
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)