Inbuilt with multi-purpose announcement bar Check here


Thread Rating:
  • 0 Vote(s) - 0 Average
  • 1
  • 2
  • 3
  • 4
  • 5
Swala ya Sunna
#1
Maana ya Swala ya Sunna (kujitolea)
Swalah ya Sunna
Swalah iliyowekwa na Sheria isiyokuwa ya lazima
Fadhla za Swalah ya Sunnah
1. Swala ya sunna ni sababu ya mja kupendwa na Mwenyezi Mungu. Imekuja kwenye hadithi Alqudusiy kwamba Mwenyezi Mungu Aliyetukuka ansema: (Haachi mja wangu kuendelea kujikurubisha kwangu kwa sunna mpaka nimpende, na ninapompenda nitakuwa ni masikizi yake ya kusikia na maangalizi yake ya kuonea na mkono wake wa kushikia na mguu wake wa kuendea, na akiniomba nitampa, na akijilinda kwangu nitamlinda) [Imepokewa na Bukhari.]
2. Swala ya sunna inaunga kasoro za faradhi. Mtume (s.a.w) amesema: (Kitu cha kwanza wanachohesabiwa kwacho Siku ya Kiyama miongoni mwa matendo ni Swala. Mwenyezi Mungu aliyetukuka, Atawaambia Malaika wake- na yeye ni mjuzi zaidi-: “Itizameni Swala ya mja wangu, je ameikamilisha au ameipunguza?” Iwapo imekamilika inaandikwa kuwa imekamilika, na ikiwa ina upungufu wa kitu, Atasema: “Tizameni, je mja wangu huyu ana sunna alizoziswali? Akiwa ana sunna, Atasema: Mkamilishieni mja wangu faradhi yake kutoka kwa sunna zake” ) [Imepokewa na Abu Daud.].
3. Swala ya sunna nyumbani ni bora zaidi
Swala ya sunna majumbani ni bora kushinda misikitini isipokuwa katika Swala ziliwekewa jamaa na Sheria kama Swala ya Tarawehe katika mwezi wa Ramadhani. Mtume (s.a.w) amesema: (Bora zaidi wa Swala ya mtu ni ile anayoiswali nyumbani kwake isipokuwa Swala ya faradhi) [Imepokewa na Bukhari.].
https://www.al-feqh.com/sw/swala-ya-sunna
Reply


Forum Jump:


Users browsing this thread: 1 Guest(s)