Page 1 of 1

KOCHA WA LIVERPOOL (KLOPP) AWAJIBU WANAOSEMA KUA SALLAH HANAFURAHA LIVERPOOL:

Posted: Thu Jan 07, 2021 7:28 am
by kanonko23
Kama ulidhani Mohammed Salah kwasasa hana furaha Liverpool, basi unajidanganya na haiko hivyo, Kocha wa Majogoo hao wa Jiji la Liverpool, Jurgen klopp amezipiga chini taarifa hizo alizoziita ni uzushi.

“Salah ana furaha, hilo ndilo jambo muhimu kwasasa, hatukupiga picha tukiwa mazoezini, ila umeona jinsi alivyokuwa akifurahi” amesema Klopp.

Salah aliyaambia magazeti ya Hispania kuwa alichukizwa kufuatia kutokuwa nahodha katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa dhidi ya Midtjyland na badala yake kitambaa cha unahodha alipewa Alex Anord.

Re: KOCHA WA LIVERPOOL (KLOPP) AWAJIBU WANAOSEMA KUA SALLAH HANAFURAHA LIVERPOOL:

Posted: Thu Jan 07, 2021 10:16 am
by Singa
Salah ameshachoka hana maajabu kabisa huyo, nadhan Sadio Mane ndio hatari zaidi kuliko salah