China kubadilisha hekta milioni 6.7 za ardhi yenye chumvi na alkali kuwa mashamba ya mpunga

kijiwe hiki ni mahususi kwa hoja na habari mbalimbali. jenga hoja na shirikisha wanakijiwe na maswala mbalimbali yahusuyo jamii yetu na dunia kwa ujumla
Post Reply
Singa
Posts: 5
Joined: Sat Jan 02, 2021 2:13 pm

China kubadilisha hekta milioni 6.7 za ardhi yenye chumvi na alkali kuwa mashamba ya mpunga

Post by Singa »

Timu ya mtaalamu maarufu wa kilimo wa China Yuan Longping leo imetangaza kuwa, inapanga kulima mpunga unaoweza kuvumilia chumvi na alkali katika hekta milioni 6.7 za ardhi yenye chumvi na alkali nchini China katika miaka 8 hadi 10 ijayo.

Timu hiyo imesema imesaini mkataba wa kuendeleza ardhi ya hekta laki 4 yenye chumvi na alkali nchini China.

Timu ya Bw. Yuan imefanikiwa kuchunguza mpunga unaoweza kuvumilia chumvi na alkali mwaka 2017, na kupata rekodi ya juu zaidi ya mavuno ya tani 12 kwa kila hekta mjini Jiangsu mwaka jana.Image

Sent from my Infinix X656 using Tapatalk

Post Reply